Jumatano 11 Juni 2025 - 23:25
Soko haramu la tiketi za ndege kwa ajili ya kuikimbia Israel

Hawza/ Idadi ya Wazayuni wanaojaribu kukimbia kutoka Palestina iliyokaliwa kwa mabavu imeongezeka kwa kiwango kikubwa. Hata hivyo, kutokana na mashambulizi ya makombora kutoka Yemen, mashirika mengi ya ndege za kigeni yamesitisha safari zao kuelekea Tel-Aviv, jambo ambalo limezusha sintofahamu katika ardhi hii inayokaliwa kwa mabavu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, gazeti la Kiebrania la "Maariv", Jumanne tarehe 10 Juni liliripoti kuwa idadi ya wahamiaji Wazayuni walioiacha Israel mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 28.

Kulingana na ripoti hiyo, zaidi ya watu 718,000 wamehama kutoka Palestina inayokaliwa kwa mabavu tangu tarehe 7 Oktoba 2023. Hata hivyo, katika miezi ya hivi karibuni, hali imekuwa mbaya zaidi kuliko hapo awali, na takwimu hizo zimepanda kwa kiasi kikubwa.

"Maariv" limeandika kuwa kufuatia mashambulizi ya makombora ya Yemen, mashirika mengi ya ndege ya kigeni yamesitisha safari zao kuelekea Tel Aviv, jambo ambalo limepelekea ongezeko kubwa la bei za tiketi za ndege.

Kwa mujibu wa ripoti za gazeti hili, Wazayuni wanajitahidi kuondoka Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa njia ya ndege, lakini idadi ya ndege zinazopatikana haikidhi wimbi hili la wahamaji wanao ikimbia Israel.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha